Saturday, December 31, 2011

NUKUU MARIDHAWA YA KUANZA MWAKA 2012

NUKUU MARIDHAWA: Uandishi wa habari kamwe hauwezi kuwa kimya hiyo ndiyo sifa na udhaifu wake.Lazima useme na useme haraka.

– HENRY ANATOLE GRUNWALD, (1922-2005)

Mhariri wa zamani wa jarida la TIME.
 “Journalism can never be silent: that is its greatest virtue and its greatest fault. It must speak, and speak immediately, while the echoes of wonder, the claims of triumph and the signs of horror are still in the air.” – Henry Anatole Grunwald
Are you interested in creative writing and do you have lot of opinions to share and you really want to live your right to freedom of speech and expression, then what/who are you really waiting for? Journalism is a field where one can express through both written and spoken words.
Journalism is for those who like to bring truth into the limelight. 

If you want to bring change in the society and want the world listen to you then this is the best job for you. Journalism is like a wielding stick on the society. Journalism is the fourth pillar of democracy.

MBEYA BROADCASTERS NETWORK INAKUTAKIA MWAKA 2012 WENYE BARAKA ZA MWENYEZI MUNGU

RAIS WA MBN GABRIEL MBWILE ANASEMA HIVI KUHUSU MWAKA 2012

As we have started 2O12 We might have haurted u unintentional or treated u unfairly in one way or another. As we learn through mistakes of others. We berg ur forgiveness  so that we can start  a new year afresh. 

Wish u all the best in 2012

WAKRISTO WATAKIWA KUWA NA MIPANGO KWA AJILI YA MWAKA 2012

Wakristo mkoani Mbeya wametakiwa kuwa na mipango kwa maisha yao ya  baadaye badala ya kutegemea kudra za Mwenyezi katika mafanikio yao.
Akizungumza katika Ijumaa ya Marafiki Meneja wa Benki ya Stanbic Tawi la Mbeya Willy Afumwisye amesema wakristo wengi wamekosa mipango katika maisha yao licha ya Neno la Mungu kuwapa ahadi kedekede.

Pia amesema wakristo wengi wamekuwa wakitegemea kuwekewa mikono na Watumishi wa Bwana ili waweze kufanikiwa kitu ambacho wakati mwingine sio sahihi isipokuwa ni uzembe wa kiakili.

Hata hivyo amesema kumtanguliza Mungu katika kila jambo ni muhimu sana kwani hakuna mafanikio bila Muumba wa Mbingu na Nchi na kuongeza kuwa anapopanga ni lazima kupanga na Roho Mtakatifu.

FOF Jijini Mbeya ni ya Pili, hufanyika kia Ijumaa ya mwisho wa mwezi. Washiriki akali ya 35 walikuwepo katika Ijumaa ya Marafiki Jijini Mbeya.

Imeandikwa na Johnson Jabir Redio Ushindi FM Desemba 30, 2011.

MBASPO SPORTS ACADEMY AYINYUKA INTER FOREST 1-0

MWAMBAMBALE CUP 2011/2012

MICHUANO ya Mwambambale imeendelea katika viwanja vya Shule  ya Msingi Mbata Jijini Mbeya kwa mechi moja leo huku ikishuhudiwa Mbaspo Sports Academy wakiikanyanga Inter Forest 1-0.

Bao hilo pekee la Mbaspo limefungwa dakika ya 80’ ya mchezo.

Desemba 30 Old Forest waligagadua Town Star 2-1

Januari Mosi 2012 Uswazi FC itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Majengo FC.

Thursday, December 29, 2011

MENEJA WA REDIO USHINDI FM MATTHEW SASALI

MENEJA WA REDIO USHINDI FM MATTHEW SASALI (KUSHOTO) ASUBUHI YA LEO KAMA ALIVYOKUTWA NA KAMERA ZA MBN MAENEO YA MAFIAT MKABALA NA MBEYA CANNIVAL AKIWA KATIKA CAR WASH YA GARI LA OFISI YAKE LAKINI HAPA WAKIWA KATIKA MAZUNGUMZO NA MDAU WA REDIO HIYO.

CHANGAMOTO YA MAFUTA JIJINI MBEYA LEO ALHAMIS

 KITUO CHA BP MWANJELWA JIJINI MBEYA LEO ASUBUHI KILIVYOKUWA

Wednesday, December 28, 2011

SAKATA LA WALIMU WA ST. FRANCIS MBEYA LACHUKUA SURA

LILE sakata la walimu wa shule ya wasichana ya Mtakatifu Fransisco wa Azizi Mbeya (St.Francis) kugomea ndani ya nyumba  limechukuwa sura mpya baada ya Serikali mkoani hapa kuingilia kati na kuliangukia kanisa Katoliki kutoifunga shule hiyo  kama ilivyotarajiwa  baada ya masista wenye asili ya kiasia wa Shirika la Mt.Karoli  Boromeo  ambao ndiyo viongozi na waendeshaji wa shule kuitwa mara moja na mama yao mkuu  kurudia haraka nchini Ubelgiji  kuhofia  kuvamiwa na walimu hao.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Abbas Kandoro akizungumza katika kikao  na viongozi wa kanisa katoliki Jimbo la Mbeya  alichokiitisha ofisini kwake jana amemsihi Askofu Evaristo Chengula wa kanisa jimbo  ambaye ndiye mmiliki wa shule hiyo kuvuta subira na kubadilisha wazo la kuifunga shule hiyo kwani serikali imeamua kuingilia katika  kulishughulikia suala hilo haraka iwezekanavyo.

“Tunampa pole Baba  Askofu  tunajuwa anaumia  na  krismas kwake imepita bure,avute subira  lakini ajuwe anashughulika na binadamu aendelee kuwa mvumilivu hasifunge shule…shule hii inatuletea sifa katika Mkoa na taifa kwa ujumla  na kutokana na ubora wa elimu inayotoa imekuwa ni tegemeo na kimbilio la wengi, wanafunzi  zaidi ya 360 wanaosoma hapo watayumba,wazazi watachanganyikiwa,nawaagiza pande zote mbili na wanasheria wenu mketi kwa pamoja na kulimaliza suala hili kwa amani na utulivu…ila siingilii masuala ya kisheria,”alisema.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa Kandoro alituma ujumbe wake ulioongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya,Evans Balama kwenda kwa Askofu Chengula kufikisha salamu hizo na kuahidi kulishughulikia tatizo hilo mapema ambapo kwa wake Askofu Chengula aliiomba serikali kulishughuliki suala hilo kabla ya januari,8 siku ya kufungua shule za bweni  kabla masista hao ambao ndiyo Meneja wa shule hawajaondoka nchini ili aweze kuwasihi  kurejea shuleni  vinginevyo ataifunga shule kutokana na kukosa  walimu na Uongozi wa   kuiendesha.

 Kwa mujibu wa maelezo ya Mkurugenzi wa idara ya elimu Jimbo Katoliki la Mbeya,Padri  Innocent sanga alisema  awali masista wa shirika la Mtakatifu Fancisco wa Asizi waliendesha shule hiyo kwa makubaliano ya mikataba mizuri na  walimu hao  kuwalipa mishahara  minono iliyofikia wastani wa Tsh.Mil.2 ,lakini baada ya kumaliza mkataba wao na kuikabidhi shule kwa Askofu Chengula,  Jimbo lilishindwa kuiendesha  kutokana na  kutumia fedha nyingi kuwalipa walimu.

“Wenzetu walikuwa na fedha nyingi lakini sisi hatuna chanzo kingine cha kuendesha shule zaidi ya kutegemea ada  kwani  shule tunaiendesha kama huduma na siyo kibiashara,tuliamua kukaa nao kuwaeleza kusudio leo la kubadilisha mikataba mipya, tuliangalia tunatumia zaidi ya Sh.Mil.548,000,000 kulipa mishahara ya walimu sawa na asilimia 76 ya mapato ya shule na Sh.Mil176,000,000 sawa na asilimia 24 ndiyo inasalia  na tunalazimika kutumia fedha za gharama ya bweni na chakula ili kufidia mishahara mikubwa  na ndiyo maana ilipofika mwaka huu tulishindwa kabisa kuiendesha shule”alisema.

Aliongeza,”Askofu aliamua kuwaeleza adhma ya kufuta mikataba mipya ya walimu wa kudumu,kulipa haki zao zote stahili kwa mujibu wa sheria,kuajiri upya walimu waliopo na wapya katika mikataba ya muda maalum na masharti mapya ilimradi yakubaliwe na mwajiri,kufuta marupurupu yote ya walimu ambayo si ya kisheria.

Alitaja marekebisho mengine ya mikataba  kuwa kulipa mishahara kadri ya ‘scheme of service and salary structure’ mpya ambayo jimbo limeandaa,kuanzisha malipo na marupurupu mapya kadri ya uwezo wa shule na kwa mwaka 2011 shule isipandishe ada kufikia Tsh.Mil.2 kama ilivyokusudia ili kuendelea kuwalipa walimu miashahara minono na badala yake walimu walipwe wastani wa Sh.600,000 na ada ibakie Sh.Mil.1.7.

Padre sanga alisema hata hivyo walimu hao hawakuwa tayari kupokea marekebisho hayo  na hivyo kanisa kuamua kuwaachisha kazi na kuwataka wahame  ifikapo Januari,28,2011 ndani ya nyumba za shule walizokuwa wakiishi kuwapisha walimu wengine wapya walioajiriwa hali ambayo ilipingwa na walimu hao kwa  kuomba hati maalum  katika baraza la nyumba kuzuia wasitokea hadi kesi yao ya msingi iliyopo Tume ya usuluhishi   kesi za ajira na kazi (CMA) itakapomalizika.

Alisema walimu hao  pia walipinga kuhama  kupitia wakili wao wa awali Mwakolo and Company kuwa watakuwa tayari kuhama wakati watakapolipwa madai yao ‘repatrition expenses’,yaani gharama za kuwarudisha makwao ambapo baada ya kila mmoja kuorodhesha madai yake katika walimu tisa zaidi ya Sh.Mil.31.9 zilipatikana na  kanisa lilikuwa tayari kuwalipa lakini baadaye waligoma na kuachana na wakili huyo.

Amewataja walimu hao wanaolidai kanisa  na idadi ya kiasi cha fedha katika mabano ni Rozalia Kimario aliyedai zaidi ya Sh.Mil.6.7,Mary Njele (Sh.Mil.6.6),Yessaya Musyani (Sh.336,000),Lenadina Kagero(Sh.263,000),Ernest Njole (Sh.332,000),Benezer Msangi (Sh.Mil.6.5),Ursula Ndeki (Sh.Mil.7.5),Agatha Nyagimba (Sh.328,000) na Simon Mapunda (Sh.Mil.3.2).

Ametaja madai mengine ya walimu ambayo kanisa  lilikuwa tayari kulipa kwa mujibu wa sheria ni pamoja na mshahara wa mwezi mmoja  badala ya notisi ambapo Askofu alikuwa tayari kuwalipa mishahara ya miezi sita,’disturbance allowances’,’severance allowance’ na ‘Certificate  of service cause of termination(Redundance)’.

“Hapo ndipo ilipoanza mivutano na walimu kulifikisha kanisa  katika baraza la ardhi na nyumba pamoja na Tume ya usuluhishi ambapo ‘order’ ilitolewa januari,17,2011 walimu walikaa katika nyumba hizo kwa kufuata amri ya baraza la ardhi na nyumba hadi kesi  ilipokwisha disemba,22 ,2011 kesi yao ilipotupiliwa mbali,na kesi nyingine  walimu waliyofungua  (CMA) kuitaka tume itamke kuwa “walimu hao hawakuachishwa kazi kihalali na waendelee na kazi”  ilitupilia mbali pia,”alisema Padri Sanga. 

Padri huyo alisema kutokana na maamuzi ya baraza la ardhi na nyumba kanisa liliiomba kampuni ya Yono auction mart & Cout broker kuwaondoa walimu hao jambo lililoleta mgongano wa maamuzi baada ya Mwenyekiti wa tume ya usuluhishi Boniphace  Nyambo kuliandikia Jeshi la Polisi hati ya kuwarudisha ndani ya nyumba majira ya saa 12 jioni jambo lililopelekea kuhoji uhalali wa Tume hiyo kuandika  ‘order’  wakati awali suala la nyumba lilishughulikiwa na   baraza la  ardhi na nyumba na kutoa hati iliyokwisha muda wake baada ya kutupilia mbali shauri hilo.

Alisema  Jeshi la polisi liligonga ukuta kupata ufunguo za kuwafungulia walimu hao ndipo walimu walipochukuwa hatua ya kuvunja makufuli ya nyumba zao na kuingia ndani ya nyumba hizo kuendelea kuishi hali ambayo iliwashtua masista ambao nao wanaishi ndani ya shule hiyo na hivyo kuhofia kuvamiwa na walimu na hivyo kuamua  kumpigia simu mama yao mkubwa huko nchini Ubelgiji ambaye aliwataka waondoke haraka na hivyo walimuaga Askofu Chengula na kuondoka  siku ya pili wakiiacha shule peke yake.

 Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hizi akiwa safarini kuelekea mkoani Iringa walipo masista wenzao wa Shirika hilo,mmoja wa viongozi wa masista hao,Sr.Sagaya alisema amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na walimu hao kutishia amani na utulivu na kwamba alilazimika usiku huo  kumpigia simu Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya,Advocate kumuelezea hali hiyo   lakini katika hatua ya kushangaza Kamanda Nyombi  alibariki kitendo hicho na kumuahidi kuwa watakuwa salama na hakutakuwa na uvunjifu wowote wa amani.

“Sisi tulijiuliza Polisi wanabariki walimu kuvunja nyumba?,lakini pili tukahoji kama walimu hao wamekaidi kumsikiliza Baba Askofu ambaye ndiyo mwajiri wao,je watatusikiliza sisi?, watakuja kutuvamia kwa maana zile sauti za nyundo zilitunyima raha na hamu ya kuendelea kuishi,tukampigia mama mkubwa Ubelgiji akasema tukimbilie kwa wenzetu Iringa tupo Iringa na amesema hali ikizidi kuwa mbaya turudi Ubelgiji,”alisema Sr.Sagaya.
Thompson Mpanji,  Redio Maria Mbeya Desemba 28, 2011

KIM JONG IL AZIKWA

Kiongozi mpya wa Korea Kaskazini anaongoza msafara wa mazishi ya baba yake Kim Jong Il, ambao unapita katika mitaa ya mji mkuu wa Pyongyang uliofunikwa na barafu na theluji. Picha za Televisheni ya taifa ya Korea Kaskazini zimemuonyesha Kim Jong Un akitembea sambamba na gari lililobeba jeneza la baba yake. 

Gari jingine lililobeba picha kubwa ya hayati Kim Jong Il lilifuatia katika msafara huo. Maelfu ya waombolezaji wamejipanga kando kando ya barabara wakivumilia baridi kali kumuaga kiongozi wao, na wanajeshi wanainamisha vichwa vyao kutoa heshima. 

Kim Jong Il alikufa kutokana na mshituko wa moyo mapema mwezi huu, na mazishi yake yatachukua muda wa siku mbili. Mara tu baada ya kifo chake, vyombo vya habari viliashiria kwamba Kim Jong Un ndiye atakayerithi madaraka ya baba yake.

KUPANDA BEI MAFUTA JIJINI MBEYA KWAIBUKWA MZOZO


Mzozo umeibuka Jijini Mbeya baina ya madereva wa magari na wamiliki wa vituo vya mafuta kufuatia wamiliki hao kuzuia mafuta kuuzwa katika vituo vyao kwa siku ya pili sasa.

Uchunguzi uliofanywa na redio Ushindi FM umebaini foleni kubwa katika baadhi ya vituo vya mafuta Jijini Mbeya  kwa magari hayo kutaka nishati hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyobainishwa na Redio hiyo yamebaini Kituo cha Mafuta cha JM kilichopo Maghorofani Jijini humo foleni kubwa ya magari hali ambayo imekuwa tofauti na siku nyingine.

Madereva wa magari hao wamenukuriwa wakisema mrundikano huo umetokana na EWURA kutangaza bei mpya za nishati hiyo, na kuongeza kuwa wanaiomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwachukulia hatua stahili wamiliki hao kwani wanachangia kukwamisha shughuli za kimaendeleo nchini.

Wamiliki wa vitu hivyo kwa upande wao wameishutumu Mamlaka husika kutokana na kushusha bei hali ambayo imewaongezea  hasara na kuongeza kuwa awali ilikuwa shilingi 2,200 na sasa ni shilingi 1,800

EWURA huwa na kawaida kila baada ya majuma mawili kubadilisha bei elekezi ya nishati hiyo kwa kila wilaya nchini Tanzania kufuatana na umbali kutoka hazina hadi kwa mteja.

*  Bei za nishati ya mafuta katika mkoa wa Mbeya kwa ujumla tangu Desemba 19, 2011

PETROL
DIESEL
KEROSENE
MBEYA
1989
2082
2065
CHUNYA
1999
2092
2074
ILEJE
2002
2096
2078
KYELA
2005
2098
2081
MBARALI
1973
2067
2049
MBOZI
1998
2092
2074
RUNGWE
1998
2091
2074

*Bei hizi zimeanza kutumika Jumatatu ya Desemba 19, 2011
      
            
Moses Mbembela na Rester Pharles Redio  Ushindi FM Desemba 28, 2011

Tuesday, December 27, 2011

AUAWA KWA KUFANYA MAPENZI NA MKE WA MTU

Watu wanne wamepoteza maisha katika matukio mawili tofauti mkoani Mbeya likiwemo la mwanaume mmoja kuuawa kwa kutuhumiwa kufanya mapenzi na mke wa mtu.

Jeshi la Polisi mkoani humo limesema tukio la kwanza limetokea  Jumatatu ya Desemba 26, mkazi wa Kabwe jijini Mbeya aliyefahamika kwa jina la Theresia Mbinili (85) alipoteza maisha baada ya gari namba T. 429 AHU aina ya Toyota Hiace kumgonga.

Taarifa hiyo imesema  kondakta wa gari hilo Joshua Laudeni (25) mkazi wa Iyunga amekamatwa na mwili wa marehemu umehifadhiwa  katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, na chanzo cha ajali hiyo  ni kondakta huyo kutosomea udereva na kuendesha bila leseni.

Tukio la pili limetokea Jumatatu ya Desemba 26, mkazi wa Ilongo wilayani Mbarali aliyefahamika kwa jina la Mbatalile Mwakilolile (70) kufa kwa kugongwa na gari namba T 881 BTT aina ya Toyota Hiace katika barabara ya Mbeya-Iringa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo imesema gari hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina moja tu la Sunday, ambaye alikimbia baada ya tukio.

Pia imesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Chimala Mission na kwamba chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi.

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limeongeza kusema, mkazi wa Ifuko wilayani Chunya aliyefahamika kwa jina la Zaina Zawadi (55) amefariki wakati akipatiwa matibabu katika Kituo cha Afya cha Mbuyuni baada ya kupigwa na mwanamke mwenzake.

Imebainika aliyempiga hadi kusababisha kifo chake ni Justa Stephen ambaye amekimbia baada ya kutenda kosa hilo, akimtuhumu marehemu kwa imani za ushirikina  na anatafutwa na Jeshi hilo kwa hatua zaidi.

Katika hatua nyingine Jeshi hilo limesema  mwanaume mkazi wa Chipaka wilayani Mbozi aliyefahamika kwa jina la Amos Siame (37) ameuawa kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali kisha kunyongwa kwa kamba ya gome la mti na kutupwa porini karibu na makaburi ya Chipaka.

Kwa mujibu wa Taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu tukio hilo iliyotolewa  imesema mwili wa marehemu umekutwa na jeraha kubwa shingoni.

Pia imeongeza kusema chanzo cha mauaji hayo ni marehemu kutuhumiwa kufanya mapenzi na mke Jacob Sikaonya (31) mkazi wa Chipaka.

Aidha watu watano wanashikiliwa na Polisi kuhusiana na tukio hilo akiwemo  Frank Sikaonya (28), Nimrodi Sikaonya, Waikunga Sikaonya na Ayub Sikaonya (18).

Imeandikwa na Rester Phares Redio Ushindi FM Mbeya Tanzania Desemba 27, 2011.

SUGU ATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO MBEYA

WANANCHI waliokumbwa na mafuriko Desemba 19 mwaka huu katika Mtaa wa Ikuti Jijini Mbeya na kusababisha kifo cha watoto wawili,  juzi wamepata msaada wa mahindi gunia 40 kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo Joseph Mbilinyi (Sugu)(Chadema).

Mbunge huyo alikabidhi msaada huo kwa Afisa Mtendaji wa Kata ya Iyunga, Adia Mwambela chini ya uangalizi wa Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu mkoa wa Mbeya Ulimboka Mwakilili ambaye alikabidhiwa jukumu la kuwagawia walengwa wa msaada huo.

Sugu alisema baada ya kusikia taarifa za mafuriko hayo akiwa nje ya mkoa, hakupenda kutoa matamko akiwa mbali na badala yake akaamua kurudi jimboni kujionea hali halisi na kusikiliza mahitaji ya wahanga na ndicho kilichomgusa kutoa msaada huo wa mahindi.

Alisema baada ya kuwatembelea wahanga wa mafuriko hayo, kwa kauli yao wenyewe walidai kuwa hitaji lao la kwanza ni chakula, kwa kuwa akiba waliyokuwa nayo ilisombwa na maji.

Sanjari na hilo alitanabaisha kuwa kwasababu yeye ni mwanamuziki, aliamua kufanya tamasha la Muziki siku ya mkesha wa krismasi, ambapo aliahidi kuwa katika kila tiketi ya kiingilio kwenye tamasha hilo iliyouzwa kwa shilingi 3000, shilingi 1000 itaelekezwa kusaidia wahanga wa mafuriko hayo.

Alisema kuwa katika tamasha hilo tiketi 1200 ziliuzwa na kufanikisha kukusanywa kwa shilingi milioni 3.6 na theluthi ya fedha hizo ikaelekezwa kwa wahanga hao kama alivyoahidi.

“Baada ya kukusanya fedha hizi hatukuona sababu yoyote ya kukodi fuso kwenda kununua mahindi sehemu nyingine nje ya eneo hili hapa wakati kuna akina mama na shangazi zetu wanauza mahindi hapa, hivyo tumeamua fedha hizi zibaki hapa hapa ili zisaidie kukuza uchumi wa eneo hili,” alisema Mbilinyi.

Pia aliwashukuru wananchi wa maeneo hayo ambao hawakukumbwa na athari za mafuriko hayo kwa kujitolea kuwasaidia wenzao walioathiriwa nyumba na mali zao kwa kuwasaidia kuokoa mali na kuwapa hifadhi wale ambao nyumba zao zilibolewa kabisa.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Iyunga, Adia Mwabela alimshukuru mbunge huyo na kudai kuwa ameonyesha mfano bora kwa viongozi wengine pia kujitokeza na kusaidia wahanga wa mafuriko hayo.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu Mkoa wa Mbeya, Ulimboka Mwakilili alisema msaada huo utawafikia walengwa kama ilivyokusudiwa na kuwa ugawaji wa msaada huo hauzingatii itikadi ya chama chochote wala kuingiliwa na Serikali.

Alisema mbali na msaada huo wa Mbunge, taasisi za dini za Kiislam na Kikristo zimejitokeza kutoa misaada ya kiutu huku Serikali kuu na Jiji la Mbeya pia wakiwa mstari wa mbele kutoa misaada hiyo lakini wafanya biashara pekee hawajajitokeza huku wakishindwa kujua kuwa walioathirika ni wateja wake.

Imeandikwa na Gordon Kalulunga Kalulunga Community Group Desemba 27, 2011

Monday, December 26, 2011

MWAMBAMBALE CUP: USWAZI YAICHAPA VIJANA FC 4-1

MWAMBAMBALE CUP


DESEMBA 26, 2011
UGA: S/M MBATA, JIJINI MBEYA

USWAZI FC               4-1                   VIJANA FC
Salim Kunga 23’,79’                                      John Jerome 54’
Shaban Adam 35’
Salum Zakaria 80’

DESEMBA 27, 2011

African Boys            1-3                   Nakivubo FC
Mando Mkumbwa 54' 
Daniel Peter 81'
Baraka Kajigiri 85'                         Joseph Haule 90'


DESEMBA 28, 2011

AL Jazeera  Vs  Stendi Kuu

*Mwenyekiti wa Mashindano Adam Hussein

ACHOMWA KIGANJA CHA MKONO NA MJOMBA WAKE

MTOTO Oscar Oliver (17) mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya amechomwa kiganja chake cha mkono wa kushoto na kaa la moto kwa kulazimishwa na mjomba wake akituhumiwa kuwa hana tabia njema.

Tukio hilo la kinyama limetokea usiku wa kuamkia siku ya sikukuu ya Krismas nyumbani kwa Andendekisye Mwakabubu (30) ambaye ndiye anayedaiwa kufanya unyama huo kwa mpwa wake akimtuhumu kuwa alitaka kumwibia.

Mwakabubu anadaiwa kumlazimisha mtoto huyo kushika kaa la moto na baada ya mtoto huyo kuungua kiganja chake alimpeleka katika kituo kidogo cha polisi cha Mwanjelwa na kumfunmgulia kesi ya wizi wa kuibiwa vitu mbalimbali ili kuweza kuficha unyama wake huo.

Baada ya kufungua kesi hiyo, askari polisi walimshikilia kijana huyo na kumpeleka katika kituo kikuu cha polisi mkoani hapa na kumweleza mlalamikaji huyo bandia kuwa alitakiwa kufika kituoni hapo kwa ajili ya mtoto huyo kupelekwa mahakamani.

Mtoto huyo alipofikishwa katika kituo hicho kikuu alikutana na askari waliopo ndani ya kitengo cha kuelimisha jamii kuhusu unyanyasaji wa kijinsi hususani kwa watoto ambao walimsikiliza mtoto huyo na hatimaye jana walimwita mpwa wake kwa ajili ya kutoa maelezo.

Mwakabubu baada ya kufika kituoni hapo na kutoa maelezo na kuulizwa kuwa nani aliyehusika na tukio hilo alishindwa kubainisha huku akisema kuwa hajui aliyemchoma huku akisahau kuwa katika maelezo yake ya awali yeye ndiye alikuwa mlalamikaji jambo ambalo liliwashawishi askari hao kumakamata na kumpeleka rumande.

Mpwa huyo wa mtoto Oscar akiwa mahabausu ya kituo hicho cha polisi, askari hao wanaunda mtandao huo wa kuelimisha jamii juu ya unyanyasaji wa kijinsia mkoani hapa hususani kwa watoto walimchukua mtoto huyo na kumpeleka Hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Mwakabubu alihojiwa na askari wa mtandao huo wakiongozwa na askari aliyefahamika kwa jina la Pudensiana Baito huku mwandishi wa habari hizi akiwa anafuatilia tukio hilo na askari huyo alipotakiwa kueleza kwa undani tukio hilo alisema kuwa yeye si msemaji wa jeshi la polisi.

KIFO CHA KHALIL IBRAHIM CHAZUA WASIWASI JIMBO LA DARFUR

  DW

Kundi kuu la waasi katika jimbo la Darfur, The Justice and Equality Movement – JEM- limethibitisha kuwa kiongozi wake aliuwawa na wanajeshi wa Sudan na likaapa kulipiza kisasi


Wakati jeshi la Sudan likisema kiongozi huyo wa waasi, Khalil Ibrahim, aliuwawa katika mapambano akijaribu kuingia kisiri hadi Sudan Kusini wiki iliyopita, kundi la waasi la JEM lilipinga, likisema aliuwawa katika shambulizi la angani, na kudai nchi za magharibi zilihusika katika shambulizi hilo.
Gazeti la Sudan Tribune lilinukuu taarifa ya kundi la JEM iliyosema tukio hilo linaashiria ushirikiano na njama ya baadhi ya nchi za eneo hilo na kimataifa na serikali ya mauaji ya kimbari katika jimbo la Darfur.

Kulingana na msemaji wa kundi hilo, ambalo lilijiondoa kitoka mpango wa amani na serikali mwaka jana, amesema kwa kufanya njama hiyo, serikali ya Sudan imefungua milango ya mauaji ya kisiasa.

Ibrahim yadaiwa alirejea kutoka nchini Libya mwaka huu, baada ya kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi, ambapo kundi la JEM lilipata msaada. Taifa jipya huru la Sudan Kusini pia linashtumiwa na serikali ya Sudan kwa kuwasaidia waasi.

Kulingana na ripoti na mikanda ya video inayoenezwa kwenye mitandao ya internet, polisi mjini Khartoum waliwatawanya wafuasi wa JEM waliojaribu kutoa rambirambi zao nyumbani kwa familia ya Ibrahim viungani mwa mji huo mkuu wa Sudan. Haijabainika ni nani atakayechukua mahala pa kiongozi wa kundi hilo la waasi ambalo aliliunda mwaka 2000.

#b#Katika mzozo wa Darfur, ambao umeendelea tangu mwaka 2003, zaidi ya watu laki tatu wameuwawa kulingana na Umoja wa mataifa, ijapokuwa serikali ya Sudan inasema idadi hiyo iko chini.

Waziri wa habari wa Sudan, Abdullah Massar, amesema kifo cha Ibrahim kinatuma ujumbe kwa makundi ya waasi kuisikia sauti ya busara na kujiunga na mchakati wa kutafuta amani. Alisema jana kuwa milango yao iko wazi na kwamba mkataba wa Doha ungali wazi.

Kifo cha Ibrahim, ambaye kila mara alitajwa kuwa kiongozi jasiri, huenda kikawa pigo kubwa kwa kundi la waasi wa JEM. Mtalaamu mkuu nchini Sudan, Alex de Waal, amesema Khalil Ibrahim alitawala kundi la JEM na kibinafsi alibaini mikakati ya kisiasa na kijeshi ya kundi hilo na hasa ndiye aliyezuia kundi hilo kufanya mazungumzo ya amani na serikali ya Sudan, hivyo kifo chake ni pigo kubwa kwa waasi hao.

Uongozi katika mji mkuu wa Khartoum utahisi kukichukulia kifo chake kwa kuzingatia kuwa uasi katika jimbo la Darfur sasa umekwisha. Wakati tishio linalotolewa na kundi la JEM bila shaka likionekana kupungua, inaweza kuwa makosa kwa serikali kudhani kuwa mgogoro wa kisiasa katika jimbo la Darfur unaweza kutatuliwa kwa urahisi.

Sunday, December 25, 2011

AIRTEL MBEYA, TANZANIA


HIVI NI ALAJI AU LAFEJI


MAJI TUNAYOKUNYWA YANA RADIOACTIVE

By Ashlee Davis, Health
This year’s spate of natural disasters has reignited the debate over the safety of nuclear energy, as well as the fears of people who worry they could be exposed to harmful radiation. (As if the recent earthquake on the East Coast wasn’t enough to rattle our nerves, it led to the automatic shutdown of two reactors at a Virginia power plant.) 
 
Fortunately, most of these fears are unfounded. Even after an earthquake caused a partial meltdown of a Japanese power plant in March, sending plumes of radiation drifting across the Pacific, G. Donald Frey, PhD, a professor of radiology at the Medical University of South Carolina, in Charleston, reassured Americans that the "very low levels" of radiation were "no reason to be concerned."

That's because the radiation was just a fraction of the so-called background radiation we absorb each year, from both natural and manmade sources. To put our newfound radiation fears in perspective, here are nine sources of everyday exposure.

POLISI WAKAMATA MTAMBO WA KUTENGENEZA NOTI BANDIA

SUMBAWANGA, RUKWA

MWANAMKE mmoja mkazi wa Bomani mjini hapa ambaye ni fundi wa kushona, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kukutwa na mtambo na vifaa vya kutengenezea noti bandia.

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Isuto Mantage aliyemtaja mtuhumiwa kuwa ni Dafrosa Ramadhani (30).

Alikamatwa usiku wa kuamkia jana, majira ya saa tano.

Akifafanua, Kamanda Mantage alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kuliwezekana baada
ya polisi kupata taarifa za siri na baada ya kupekuliwa nyumbani kwake, alikutwa na mabunda
manne ya karatasi zilizokatwa mfano wa noti.

Kwa mujibu wa Mantage, mama huyo pia alikutwa na mabunda mengine manne yenye
karatasi nyeusi mfano wa dola ya Kimarekani.

Ilidaiwa kuwa kila bunda moja la karatasi nyeusi lilikuwa limewekewa alama kuonesha kuna dola za Kimarekani 100,000, sawa na Sh milioni 170.

Mantage aliendelea kuorodhesha vifaa vingine kuwa ni pamoja na kasha moja lenye chupa nne
zenye dawa ya kusafishia fedha hizo za Marekani na chupa nne tupu za dawa hizo.

Pia mwanamke huyo alitajwa kukutwa na makasha mawili na paketi kumi za dawa ambazo hazijajulikana zikidhaniwa kutumika katika shughuli hiyo ya kutengeneza noti bandia pia alikutwa na raba na gundi ya karatasi.

Alidai kuwa mtuhumiwa bado anaendelea kuhojiwa na polisi ambapo atafikishwa mahakamani
mara tu uchunguzi wa awali utakapokamilika.

Thursday, December 22, 2011

KATIBU MWENEZI WA CCM AOMBOLEZA KUFA KWA KIM JONG IL

 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) CCM, Itkadi na Uenezi Nape Nnauye akitia saini kitabu cha maombolezo kifo cha Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Il, kwenye ubalozi wa nchi hiyo uliopo Mikocheni, Dar es Salaam. 
Picha na Bashir Nkoromo.

ZAIDI YA WATU 50 WAUAWA NCHINI IRAQ

DW
Huku viongozi wa kisiasa wa Iraq wakiwa katika mgogoro wa kimadaraka na kisheria, inaonekana vurugu zinazotokana na madhehebu zimeanza tena nchini humo, baada ya makumi ya watu kuuawa hivi leo katika miripuko ya mabomu. 

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya Iraq, jumla ya mashambulizi 11 yanayoonekana kupangwa vyema, yamewauawa kwa uchache watu 50 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 170. Mashambulizi hayo yamefanywa asubuhi ya leo wakati watu wakikimbilia kazini katika kila kona ya mji mkuu, Baghdad.

 

Maafisa wa usalama wamesema maeneo yaliyoshambuliwa ni Allawi, Bab al-Muatham na Karrada yaliyo katikati ya Baghdad, Adhamiyah, Shuala na Shaab yaliyo upande wa kaskazini, Jadriyah upande wa mashariki, Ghazaliyah upande wa magharibi na Al-Amil na Dura kwa upande wa kusini.


Mauaji haya yamefanyika katika wakati wanasiasa nchini Iraq wakilumbana juu ya hati ya kukamatwa kwa makamo wa rais, Tariq al-Hashimi, ambapo Waziri Mkuu Nouri al-Maliki ameitaka mamlaka ya jimbo la Kurdi, kumkabidhi kiongozi huyo wa Kisunni kwa serikali yake, kukabiliana na mashitaka ya kupanga mashambulizi dhidi ya viongozi wa serikali.