Friday, January 27, 2012

RAIS WA MBEYA BROADCASTERS NETWORK APATA MTOTO

 MTOTO WA KWANZA WA RAIS WA MBN JINA LAKE NI CATHERINE MBWILE

 GABRIEL MBWILE AKITABASAMU NYUMBANI KWAKE NA MKEWE MAENEO YA AIRPORT JIJINI MBEYASHEMEJI MTU NAYE HAKUKOSA KUJA KUMUONA KICHANGA HUYO NA KUMTUNZA KWA VITU MBALIMBALI

Sunday, January 15, 2012

MAELFU WAOMBOLEZA KIFO CHA REGIA

 Rais Jakaya Kikwete akijiunga na waombolezaji katika msiba wa Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA) Mh Regia Mtema leo January 15, 2012 nyumbani kwa marehemu Tabata jijini Dar es salaam ambako Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda, Spika Anne Makinda na Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe walikuwapo.

 Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mwenyekiti wa Chama Cha CHADEMA Mh Freeman Mbowe wa tatu kutoka kulia pamoja na jamaa wa Marehemu Regia Mtema.
Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda katikati pamoja na Spika wa Bunge Mh. Anne Makinda.

PICHA NA IKULU YA TANZANIA

BAN KI MOON AMUONYA ASSAD

DW
Miezi  kumi  baada   ya  ghasia   kuzuka  nchini  Syria , katibu  mkuu  wa  umoja  wa  mataifa  Ban Ki-moon ametaka   rais  wa  Syria  Bashar al-Assad  kuacha kuwauwa  watu  wake.
Ban  alikuwa  akizungumza  katika  mkutano  mjini  Beirut kuhusu  demokrasia   katika  mataifa  ya  Kiarabu. Wakati huo  huo , Assad  ametangaza  msamaha  kwa  makosa yaliyofanywa  wakati  wa  machafuko  nchini  humo. Hatua hiyo  inahusu  pia  ukiukaji  wa  sheria  katika maandamano  ya  amani , kuwa  na  silaha  kinyume  na sheria  na  kulikimbia  jeshi. Kuachiliwa  kwa   wafungwa  ni moja  kati  ya  masharti  muhimu   ya  mpango  wa  mataifa ya  Kiarabu  ulioidhinishwa  na  Syria  hapo  Novemba mwaka  jana  kumaliza  mzozo  wa  nchi  hiyo, ambao umoja  wa  mataifa  unakadiria  kuwa  umesababisha  watu 5,000  kupoteza  maisha  yao. Jana  Jumapili ,  kiasi  ya watu  21  wameuwawa.

IKULU YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA CHADEMA KUFUATIA KIFO CHA MHESHIMIWA REGIA MTEMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Mbowe, kuomboleza kifo cha Mbunge wa Viti Maalum wa chama hicho, Mheshimiwa Regina Mtema.

Mheshimiwa Mtema ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Waziri Kivuli wa Kazi na Ajira amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Ruvu, Mkoa wa Pwani, asubuhi ya leo Jumamosi, Januari 14, 2012.

Katika salamu zake, Mheshimiwa Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Mbowe kuwa amesikitishwa na kuhuzunishwa na habari za kifo cha mbunge huyo ambaye amepoteza maisha akiwa bado kijana na kwamba pigo hilo siyo kwa Chama cha Chadema peke yake bali ni kwa taifa zima.

“Nimepokea kwa masikitiko na huzuni nyingi habari za kifo cha Mheshimiwa Mtema katika ajali ya gari. Siyo kwamba ajali hii imechukua maisha ya kijana bali imelinyang’anya taifa mbunge hodari, na kwa hakika, kifo chake siyo tu ni pigo kwa chama chako cha CHADEMA bali ni pigo kwa sote na kwa taifa letu kwa jumla. Nakutumia wewe binafsi, chama chako na wanachama wake salamu za dhati ya moyo wangu kuomboleza kifo na msiba huu mkubwa.”

“Napenda ujue kuwa niko nanyi katika msiba huu. Napenda vile vile uniwasilishie salamu zangu za rambirambi za dhati kabisa kwa wana-familia, ndugu na jamaa wa marehemu Mheshimiwa Mtema. Wajulishe kuwa nimepokea habari hizo kwa uchungu mwingi na kuwa moyo wangu uko nao katika wakati huu mgumu wa maombolezo, “ amesema Mheshimiwa Rais na kuongeza.

“Aidha, wajulishe kuwa nawaombea kwa Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, awajalie uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu kwa sababu yote ni mapenzi yake. Naungana nawe, Mheshimiwa Mwenyekiti, na wanafamilia wa marehemu kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke pema peponi roho ya Mheshimiwa Regina Mtema. Amen.”

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu,
DAR ES SALAAM.

14 Januari, 2012
MELI YAPINDUKA


DW

Nahodha wa meli ya abiria atiwa korokoroni nchini Italia ,huku uchunguzi ukifanyika juu ya madai ya kuuwa bila kukusudia.

Vyombo  vya  habari  nchini  Italia  vimeripoti   jana  kuwa nahodha  wa  meli  ya  abiria ,inayojulikana  kama  Costa Concordia , ambayo ilipinduka katika  pwani  ya  Toscana , nchini  Italia, ikiwa  na  abiria  4,000  amekamatwa  wakati uchunguzi   unafanyika  juu  ya  madai   ya  kuuwa  bila kukusudia  na  kuitelekeza  meli  yake. 

 

Meli  hiyo  ya  abiria  iligonga  mwamba  baharini  na kusababisha  tundu  la  mita  70  hadi  100  katika  eneo lake  la  mbele , muda  mfupi  baada  ya  kuanza  safari siku  ya  Ijumaa  kutoka   bandari  ya  Civitavecchia  karibu na   Rome. 
Kiasi  ya   watu  42  wamejeruhiwa ,  ambao watu  wawili   hali  zao  ni  mbaya  na  wengine  41  ambao ni  miongoni  mwa  watu  waliokuwa  ndani  ya  meli  hiyo wakiwa  hawajulikani  waliko. 
Meli  hiyo  ilikuwa  ikielekea katika  bandari  ya  Savona  kaskazini-magharibi  ya  Italia na  ilitarajiwa  kusimama  katika  bandari  za  Marseille nchini  Ufaransa  pamoja  na  Barcelona  nchini  Hispania.

MSIKILIZE MBUNGE WA VITI MAALUM DK MARRY MWANJELWA JUU YA KUBORESHA MIUNDOMBINU

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya Dr Marry Mwanjelwa(kushoto) akipewa utaratibu na maelezo kutoka kwa Muuguzi mata baada ya kutembelea wodi la akina Mama Wajawazito.


HITIMISHO:- 
Mahojiano ya moja kwa moja kati ya Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Mbeya Dk Marry Mwanjelwa na Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Bomba FM Mbeya DJ Imma Boy, Kuhusiana na jinsi ya kutatua changamoto za ubovu wa Miundombinu na itikadi za kisiasa zinazoukabili Mkoa wa Mbeya.


Hata hivyo Bi Mwanjelwa alitoa pongezi kwa Bomba FM, 104.0 Mhz kwa kufuata maadili ya uhabarishaji pasipo ubaguzi au kuunga mkono upande fulani.

MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMALIZA ZIARA KWA MAFANIKIO

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya Dokta Mary Mwanjelwa akizungumza na wananchi wa soko la sido Mwanjelwa jijini Mbeya, ataka watendaji wabovu kuondolewa ili kuweka heshima kwa serikali.
  Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Mbeya Dk Mary Mwanjelwa akihutubia wananchi katikati ya madimbwi ya maji ya mvua  huku akisisitiza kuwa ataenda kumwona mkurugenzi wa jiji la mbeya na kumwomba aje afukie madimbwi hayo huku wananchi wakimshangilia kwa ahadi hizo.
*****

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya Dokta Mary Mwanjelwa amehitimisha ziara yake ya siku nne katika jimbo la Mbeya Mjini, kwa kutembelea kata zote 36 na kuzungumza na wananchi. kupokea kero mbalimbali zinazowakabili pamoja na mchakato wa katiba.

Akizungumzia kero ya barabara jijini Mbeya linashughulikiwa kwa ukaribu kwani Mkandarasi ameshapatikana hivyo barabara ya kilometa 29 za kiwango cha lami zitajengwa, ili kuondoa adha wanazopata wananchi katika usafiri.

Hata hivyo amesisitiza wananchi mkoani Mbeya kuwasilisha kero zao kwake ili kuzifikisha kwa Idara husika, badala ya kukaa na kunung'unika ili waweze kupatiwa majibu sahihi.
Wakati huohuo amezitaka tofauti za kisiasa kuwekwa pembeni ili kuijenga Mbeya yenye mshikamano badala ya kusikia majanga yakiwemo moto na mafuriko ambayo yamerudisha nyuma maendeleo ya mkoa.

Dokta Mwanjelwa ameongeza kuwa amewataka viongozi kutimiza ahadi zao ili kuleta imani kwa wananchi.

KIKONGWE ABAKA - MBEYA

Kikongwe aitwaye Asagwile Kihaka (78) mkazi wa Kata ya Ghana jijini Mbeya, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kubaka mwanafunzi wa darasa la saba (12) (jina lina limehifadhiwa), katika shule ya msingi Mbata jijini hapa.

Mtuhumiwa alitenda kosa hilo Desemba 14, mwaka uliopita nyumbani kwake baada ya kumrubuni mtoto huyo kwa kumtuma aende kununua kuni za shilingi 1,000 na kuagiza ampelekee nyumbani kwake, ndipo alipochukua jukumu la kumbaka mtoto huyo hadi kuzirai.

Binti huyo ambaye mpaka sasa hajaweza kusema kwa kinywa hadi jumapili ya Januari 8, mwaka huu ambapo alifanyiwa maombi katika kanisa la PHM lililopo jijini hapa, ambapo aliweza kuzungumzia tatizo hilo kwa maandishi na kudai kuwa mzee Kihaka ndiye aliyemtendea unyama huo.

Uchunguzi uliofanywa na Hospitali ya wazazi Meta umebaini kuwa binti huyo mara kadhaa amefikishwa hospitalini na kupatiwa matibabu ya homa, lakini hakuzungumza kilicho msibu hadi pale aliupokuja kuandika kuwa kabakwa na mzee huyo na kugundulika sehemu za siri zikiwa na michubuko na vidonda hali ambayo ilithibitishwa kuwa kaingiliwa na mwanaume.

Hata hivyo wananchi waliitisha mkutano wa hadhara kutokana na kuchoshwa na vitendo vya Mzee Kihaka ambapo imetajwa kuwa ni tukio la tatu la mzee huyo kutenda na viongozi wa Kata ya Ghana kumfumbia macho.

Mzee Kihaka alikamatwa Januari 2, mwaka huu na kupelekwa Kituo cha Polisi cha Kati cha Mkoa, ambapo Mtendaji wa Kata hiyo aliwasilisha barua ya kumwekea dhamana hali iliyopingwa na wakazi na kuamua kuitisha mkutano wa hadhara Januari 13 kwa hofu alikamatwa na kurudishwa mahabusu siku moja kabla ya mkutano huo wa hadhara Januari 12.

Wakati huohuo siku ya mkutano wa hadhara Diwani wa Kata hiyo Bwana Anjelo Chavaligino hakuhudhuria mkutano huo hali iliyopelekea kuleta hasira kwa wananchi hao na kisha kumtafuta hadi kumpata na kumleta kwenye mkutano huku akizomewa na wananchi wengine walienda kupiga mawe vioo vya nyumba ya Mzee Kihaka.

Mtandao huu umeshuhudia familia ya mzee huyo ikiangua kilio baada ya kunusurika na mawe hayo.

Jeshi la polisi mkoani Mbeya lilifika eneo la tukio na kuzuia ghasia hizo na Diwani wa kata hiyo Bwana Chavaligino ameahidi kuitisha mkutano ili kujadili mstakabali wa Mzee Kihaka, huku kwa upande wao wananchi wamemtaka Mzee huyo na familia yake kuhama eneo hilo.

Thursday, January 5, 2012

WASOMALIWA WAKUTWA WAKIWA WAFU

Wahamiaji 20 Wasomali walipatikana wamekufa wiki iliyopita mashariki mwa Tanzania. Duru za polisi zimeeleza jana kuwa huenda walitupwa kichakani kutoka kwenye lori la mfanyabiashara magendo baada ya kukosa hewa  ya kutosha na  kufariki. 
Kamanda wa jeshi la polisi wa mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo amesema wanafanya uchunguzi na kisha hicho  na watatoa  taarifa  baadaye, lakini miongoni mwa waliouwawa ni wanawake watatu. Polisi wamesema wahamiaji hao wanadhaniwa walikuwa njiani kwenda Zambia au Afrika Kusini na walipatikana katika sehemu tofauti kando ya barabara kati ya Desemba 26 mwaka jana na Januari mosi mwaka huu. Maelfu ya Wasomali huikimbia nchi yao iliyokabiliwa na baa la njaa kila mwezi, baadhi wakielekea kambi za wakimbizi katika nchi jirani za Kenya na Ethiopia na wengine kwenda kutafuta ajira katika mataifa mengine kupitia msaada wa wafanyabiashara wa magendo.

JANUARI MOSI 2012 NA MBN

UONGOZI WA MBN ULIITWA NA KITUO CHA REDIO ROCKFM KINACHORUSHA MATANGAZO YAKE KUTOKA MBEYA TANZANIA KWA NYANDA ZA JUU KUSINI KUJADILI MASUALA YA KIMICHEZO. RAIS WA MTANDAO HUO WA WATANGAZAJAI MBEYA GABRIEL MBWILE, WAZIRI MKUU WA MBN JOHNSON JABIR NA KATIBU OFISI YA WAZIRI MKUU YAHYA MOHAMMED.
MTANGAZAJI NA MWANACHAMA WA MBN FRANK MAHAMILA NA MOSES PHILIP WAKIW A NDANI YA STUDIO.
RAIS WA MBN GABRIEL MBWILE NA MTANGAZAJI WA REDIO BOMBA FM MBEYA
JOHNSON JABIR NA YAHYA MOHAMMED
RAIS WA MBN AKITETA JAMBO NA HAROUB (KATIKATI) AKIWA NA KATIBU WA MBN OFISI YA WAZIRI MKUU YAHYA MOHAMMED
JUMA MPERA NJE YA STUDIO ZA ROCK FM ZILIZOPO FOREST MPYA