| Nyoka amtoa baru mbunge | ||||||||||||||||||||||||||
|
NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri, alitimua mbio kunusuru maisha yake na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). |
||||||||||||||||||||||||||
| Mwanri
alikuwa mgeni rasmi kwa ajili ya kuendesha harambee ya kujenga Kanisa
la Kilingi, akiwa na mkewe meza kuu, aliwashangaza waumini alipokimbia
akiwa amenyanyua mikono juu huku akitamka maneno ya “shindwa kwa Jina
la Yesu wewe shetani, shetani shindwa kwa Jina la Yesu,” na wageni
wengine waalikwa wakianguka chini wakijiokoa. Hali hiyo ilitokea baada
ya nyoka kutoka kusikojulikana kuingia kanisani huku Naibu Waziri
akijiandaa kuendesha harambee ya ujenzi wa Kanisa. Waumini
walikimbizana na kiumbe huyo kwa mawe na viti bila kujali kama walikuwa
ibadani, huku Askofu na wachungaji wengine wakiendelea kusali na
waumini kutakiwa kurejesha utulivu katika ibada. Tukio hilo lilitokea katika ibada ya saa nne iliyokuwa ikiongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shao, ambayo pia ilikuwa ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo. Hata hivyo, jitihada za waumini za kumkimbiza nyoka huyo kutaka kumwua hazikufanikiwa, baada ya kutoweka asionekane tena, jambo lililoacha simulizi la ni kwa jinsi gani alifika mahali hapo. “Inashangaza sana kwani lazima ujiulize alifikafikaje hapo mbele, wakati nyuma yangu kulikuwa na watu wengi...alikuwa na hasira sana, kwani alikuwa tayari kung'ata, kwa kweli hadi sasa mimi sielewi ni mambo gani haya,” alisema Mwanri.
| ||||||||||||||||||||||||||
Sunday, February 12, 2012
ASKOFU ASHINDWA NGUVU NA SHETANI AKIWA KANISANI
AUAWA KISHA MWILI WAKE KUCHARANGWA KAMA MNYAMA AKIWA KILABUNI
MBOZI
NI tukio la kusikitisha na kuleta simanzi ambalo limetokea
katika familia ya Mzee Jackson Mwashiuya(78) na wakazi wa mtaa wa Ichenjezya mjini Vwawa wilayani Mbozi mkoani
Mbeya baada ya mjukuu wake Dominick Mwashiuya kutekwa na watu wasiofahamika
kisha kumuua kikatili kwa kukatwakatwa viungo vyake vya mwili na kutelekezwa
katika chumba cha kuuzia pombe za kienyeji.
Tukio hiolo la Mauaji ya kusikitisha limetokea Ijumaa majira
ya saa 11 jioni ambapo marehemu aliitwa na mmoja wa wanawake wanaouza pombe ya
Ulanzi katika kilabu maarufu ya pombe za kienyeji inayofahamika kwa jina la ’Kwa
Jimmy’ambapo muda mfupi baadaye marehemu alikutwa akiwa amekufa huku mwili wake
ukiwa umetapakaa damu.
Mwili huo wa marehemu ulikutwa katika chumba kilichoandikwa ‘Ikumbilo
Kilabu’ ambapo muuzaji wa chumba hicho mwanamke aliyefahamika kwa jina moja la
Nampashi alitoweka na watu wasiofahamika wanaodaiwa kuhusika na mauaji hayo.
Babu wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Mzee Jackson Mwashiuya
alisema kuwa, majira ya saa 11 jioni
alikutana na mwanaye aliyefahamika kwa jina la Maria ambapo muda mfupi baadaye
marehemu ambaye ni mjukuu wake wa mtoto wa kiume alikuja kwa ajili ya kumsalimia shangazi yake.
Mzee Mwashiuya alisema kuwa wakati mjukuu wake akisalimiana
na shangazi yake mara alifika mwanamke anayeuza ulanzi katika chumba
kilichoandikwa ‘Ikumbilo Kilabu’ anayefahamika kwa jina moja la Nampashi ambaye
alimuita marehemu na kwenda naye katika chumba anachouzia pombe aina ya ulanzi.
Alisema kuwa yeye aliondoka na kuingia katika chumba kingine
kilichopo Kilabuni hapo ambapo alijumuika na watu wengine katika burudani ya
kunywa pombe za kienyeji bila kujua kinachoendelea katika chumba cha pili
ambacho kimepakana na chumba walichokuwa wameketi wao.
‘’Sikujua kinachoendelea katika chumba cha pili nilikaa na
wazee wenzangu tunakunywa komoni, baadaye walifika watu kutueleza kuwa kuna mtu
ameumizwa chumba cha pili…wote tulitoka ndani na kusimama nje ya chumba
alichofia marehemu bila kujua ni nani aliyemo humo ndani,’’alisema Mzee
Mwashiuya.
Alisema kuwa walichungulia katika chumba hicho na kuona miguu
na damu ikiwa inachuruzika na kwamba kwa kuwa chumba kilikuwa na giza
hawakuweza kuutambua vyema mwili wa marehemu kwa wakati huo.
Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa mtaa wa Ipanga ambao
umepakana na mtaa wa Mpakani lilipotokea tukio Bw.Joseph Lwenje alisema kuwa
mara baada ya kupata taarifa za tukio hilo aliingia katika chumba hicho na
kumulika kwa kurunzi ambapo alikutana na dimbwi la damu huku mwili wa marehemu
ukiwa na majeraha makubwa.
Alisema kuwa alitoa taarifa kwa Ofisa Mtendaji wa mtaa wa
Bw.Tuliani Mwahalende ambaye aliondoka pamoja na mmoja wa wazee wa kamati
ya ulinzi na usalama ya mtaa huo
Bw.Herman Mpinga hadi kituo cha Polisi na kutoa taarifa za tukio hilo na askari polisi walifika eneo hilo na kuukagua
mwili wa marehemu ndipo ilipofahamika kuwa aliyeuawa ni mjukuu wa Mzee
Mwashiuya.
Kwa upande wake baba wa marehemu Bw.Richard Mwashiuya alisema
kuwa alifika eneo la tukio muda mfupi mara baada ya kusikia minong’ono ya
kuwepo mtu ndani ya chumba alichofia lakini hakujua kama aliyeuawa kuwa ni
mwanaye ambaye ni mtoto wa kwanza kati ya watoto wake sita.
Alisema kuwa mara baada ya kutokea mauaji hayo kumeibuka tetesi kuwa kijana wake alikuwa akishiriki mapenzi na
mwanamke anayeuza pombe za kienyeji ambapo pia inadaiwa kuwa mwanamke huyo
alikuwa na mwanaume mwingine ambaye pia alikuwa akihusiana naye kimapenzi.
Baba mzazi wa marehemu alisema kuwa walishiriki katika
kuukagua mwili wa marehemu katika hospitali ya wilaya ya Vwawa ulikohifadhiwa
na kubaini majeraha makubwa ya kukatwa na kitu chenye ncha kali ambapo viganja
vya mikono yake na vidole viliachana huku sehemu ya fuvu lake la kichwa ikiwa
imefumuka kiasi cha kuonekana ubongo.
Alisema mazishi ya kijana wake yalifanyika katika makaburi ya
Isangu yaliyopo Vwawa wilayani Mbozi majira ya saa tisa alasiri.
Aidha kufuatia mauaji hayo kamati ya ulinzi ya mitaa miwili
ya Mpakani na Ipanga ilikusanyika kujadili tukio hilo na kufikia uamuzi wa
kufunga Kilabu hicho cha pombe za kienyeji kutokana na kuonekana kuwa eneo hilo
limekuwa ni chanzo cha uhalifu.
Akizungumzia kufungwa kwa Kilabu hicho Kaimu Mwenyekiti wa
Mtaa wa Mpakani Bw.Danford Mhema alisema kuwa kamati ya ulinzi na usalama ya
mtaa iliketi na kujadili na hatimaye kugundua kuwa Kilabu hicho mbali na kuuza
pombe za kienyeji ni danguro la ngono na uvutaji wa dawa za kulevya ambalo pia
linaficha wahalifu.
Alisema kuwa eneo hilo pia ni maarufu kwa uchezaji wa kamari
ambapo pia Kilabu hicho kinakesha hadi usiku wa manane jambo ambalo limekuwa
kero kwa wakazi wa maeneo hayo huku mmiliki wa eneo hilo Bw.Jimmy Mwamlima
akishindwa kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyofanyika katika Kilabu chake.
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na linafanya uchunguzi kuwanasa wauaji ili kuwafikisha mikononi mwa
sheria.
Friday, January 27, 2012
RAIS WA MBEYA BROADCASTERS NETWORK APATA MTOTO
MTOTO WA KWANZA WA RAIS WA MBN JINA LAKE NI CATHERINE MBWILE
GABRIEL MBWILE AKITABASAMU NYUMBANI KWAKE NA MKEWE MAENEO YA AIRPORT JIJINI MBEYA
SHEMEJI MTU NAYE HAKUKOSA KUJA KUMUONA KICHANGA HUYO NA KUMTUNZA KWA VITU MBALIMBALI
Sunday, January 15, 2012
MAELFU WAOMBOLEZA KIFO CHA REGIA
Rais Jakaya Kikwete
akijiunga na waombolezaji katika msiba wa Mbunge wa Viti Maalumu
(CHADEMA) Mh Regia Mtema leo January 15, 2012 nyumbani kwa marehemu
Tabata jijini Dar es salaam ambako Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda, Spika
Anne Makinda na Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe walikuwapo.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mwenyekiti wa Chama Cha CHADEMA Mh
Freeman Mbowe wa tatu kutoka kulia pamoja na jamaa wa Marehemu Regia
Mtema.
Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda katikati pamoja na Spika wa Bunge Mh. Anne Makinda.
PICHA NA IKULU YA TANZANIA
BAN KI MOON AMUONYA ASSAD
DW
Miezi kumi baada ya ghasia kuzuka nchini Syria ,
katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon
ametaka rais wa Syria Bashar al-Assad kuacha
kuwauwa watu wake.
Ban alikuwa akizungumza katika mkutano mjini Beirut
kuhusu demokrasia katika mataifa ya Kiarabu. Wakati
huo huo , Assad ametangaza msamaha kwa makosa
yaliyofanywa wakati wa machafuko nchini humo. Hatua
hiyo inahusu pia ukiukaji wa sheria katika
maandamano ya amani , kuwa na silaha kinyume na
sheria na kulikimbia jeshi. Kuachiliwa kwa wafungwa ni
moja kati ya masharti muhimu ya mpango wa mataifa
ya Kiarabu ulioidhinishwa na Syria hapo Novemba
mwaka jana kumaliza mzozo wa nchi hiyo, ambao
umoja wa mataifa unakadiria kuwa umesababisha watu
5,000 kupoteza maisha yao. Jana Jumapili , kiasi ya
watu 21 wameuwawa.
IKULU YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA CHADEMA KUFUATIA KIFO CHA MHESHIMIWA REGIA MTEMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kiongozi wa
Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Mbowe, kuomboleza kifo cha Mbunge
wa Viti Maalum wa chama hicho, Mheshimiwa Regina Mtema.
Mheshimiwa Mtema ambaye pia alikuwa Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Chadema na Waziri Kivuli wa Kazi na Ajira amefariki
dunia katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Ruvu, Mkoa wa Pwani,
asubuhi ya leo Jumamosi, Januari 14, 2012.
Katika salamu zake, Mheshimiwa Rais
Kikwete amemwambia Mheshimiwa Mbowe kuwa amesikitishwa na kuhuzunishwa
na habari za kifo cha mbunge huyo ambaye amepoteza maisha akiwa bado
kijana na kwamba pigo hilo siyo kwa Chama cha Chadema peke yake bali ni
kwa taifa zima.
“Nimepokea kwa masikitiko na huzuni nyingi
habari za kifo cha Mheshimiwa Mtema katika ajali ya gari. Siyo kwamba
ajali hii imechukua maisha ya kijana bali imelinyang’anya taifa mbunge
hodari, na kwa hakika, kifo chake siyo tu ni pigo kwa chama chako cha
CHADEMA bali ni pigo kwa sote na kwa taifa letu kwa jumla. Nakutumia
wewe binafsi, chama chako na wanachama wake salamu za dhati ya moyo
wangu kuomboleza kifo na msiba huu mkubwa.”
“Napenda ujue kuwa niko nanyi katika msiba
huu. Napenda vile vile uniwasilishie salamu zangu za rambirambi za
dhati kabisa kwa wana-familia, ndugu na jamaa wa marehemu Mheshimiwa
Mtema. Wajulishe kuwa nimepokea habari hizo kwa uchungu mwingi na kuwa
moyo wangu uko nao katika wakati huu mgumu wa maombolezo, “ amesema
Mheshimiwa Rais na kuongeza.
“Aidha, wajulishe kuwa nawaombea kwa
Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, awajalie uvumilivu na subira katika
kipindi hiki kigumu kwa sababu yote ni mapenzi yake. Naungana nawe,
Mheshimiwa Mwenyekiti, na wanafamilia wa marehemu kumwomba Mwenyezi
Mungu aiweke pema peponi roho ya Mheshimiwa Regina Mtema. Amen.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu,
DAR ES SALAAM.
14 Januari, 2012
MELI YAPINDUKA
DW
Nahodha wa meli ya abiria atiwa korokoroni nchini Italia ,huku uchunguzi ukifanyika juu ya madai ya kuuwa bila kukusudia.
Vyombo vya habari nchini Italia vimeripoti jana kuwa nahodha wa meli ya abiria ,inayojulikana kama Costa Concordia , ambayo ilipinduka katika pwani ya Toscana , nchini Italia, ikiwa na abiria 4,000 amekamatwa wakati uchunguzi unafanyika juu ya madai ya kuuwa bila kukusudia na kuitelekeza meli yake.
Meli hiyo ya abiria iligonga mwamba baharini na kusababisha tundu la mita 70 hadi 100 katika eneo lake la mbele , muda mfupi baada ya kuanza safari siku ya Ijumaa kutoka bandari ya Civitavecchia karibu na Rome.
Kiasi ya watu 42 wamejeruhiwa , ambao watu wawili hali zao ni mbaya na wengine 41 ambao ni miongoni mwa watu waliokuwa ndani ya meli hiyo wakiwa hawajulikani waliko.
Meli hiyo ilikuwa ikielekea katika bandari ya Savona kaskazini-magharibi ya Italia na ilitarajiwa kusimama katika bandari za Marseille nchini Ufaransa pamoja na Barcelona nchini Hispania.
Subscribe to:
Posts (Atom)













