Sunday, February 12, 2012

KIFO CHA MWANAMUZIKI WHITNEY IWE FUNDISHO KW WASANII WANAENDEKEZA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA

Whitney Houston akiwa jukwaani

Mwanamuziki Whitney Houston afariki

Mwanamuziki mashuhuri wa nchini Marekani Whitney Houston ameaga dunia. Polisi mjini Los Angeles wamesema Whitney ambaye alikuwa na umri wa miaka 48, amekutwa amekufa katika hoteli iliyopo mtaa wa Beverly Hills. 

Habari za kifo cha nyota huyo zimekuja wakati ulimwengu wa muziki ukijiandaa kwa sherehe za tuzo ya Grammy leo Jumapili, na pia saa chache kabla ya tafrija ya chakula kwenye hotel ambapo marehemu Whitney Houston amepatwa na mauti.

Afisa wake wa habari Kristen Foster ambaye alikuwa wa kwanza kutangaza kifo hicho hakuelezea chanzo cha kifo chake. Hata hivyo katika miaka ya hivi Karibuni mwanamuziki huyo amekuwa akisumbuliwa na athari za matumizi ya madawa ya kulevya.


Muziki wa Whitney Houston aliuza albamu zaidi ya milioni 170
Muziki wa Whitney Houston aliuza albamu zaidi ya milioni 170

Whitney Houston alijipatia Umaarufu mkubwa katika miaka ya 1980 na 1990, kwa nyimbo zilizovuma kama  ''How will I Know'', ''Saving all my Love for You'' na ''I will always Love You''. Alishiriki pia katika uwanja wa uigizaji na kuwa katika filamu mashuhuri ya ''Bodyguard''

Wakati wa umaarufu wake Whitney Houston alishinda tuzo sita za Grammy. 

Magwiji wa muziki wametoa rambi rambi zao kupitia mitandao ya kijamii, wakimueleza Bi Houston kama mtu ambaye hatasahaulika katika fani ya Muziki.

No comments:

Post a Comment