Sunday, January 15, 2012

BAN KI MOON AMUONYA ASSAD

DW
Miezi  kumi  baada   ya  ghasia   kuzuka  nchini  Syria , katibu  mkuu  wa  umoja  wa  mataifa  Ban Ki-moon ametaka   rais  wa  Syria  Bashar al-Assad  kuacha kuwauwa  watu  wake.
Ban  alikuwa  akizungumza  katika  mkutano  mjini  Beirut kuhusu  demokrasia   katika  mataifa  ya  Kiarabu. Wakati huo  huo , Assad  ametangaza  msamaha  kwa  makosa yaliyofanywa  wakati  wa  machafuko  nchini  humo. Hatua hiyo  inahusu  pia  ukiukaji  wa  sheria  katika maandamano  ya  amani , kuwa  na  silaha  kinyume  na sheria  na  kulikimbia  jeshi. Kuachiliwa  kwa   wafungwa  ni moja  kati  ya  masharti  muhimu   ya  mpango  wa  mataifa ya  Kiarabu  ulioidhinishwa  na  Syria  hapo  Novemba mwaka  jana  kumaliza  mzozo  wa  nchi  hiyo, ambao umoja  wa  mataifa  unakadiria  kuwa  umesababisha  watu 5,000  kupoteza  maisha  yao. Jana  Jumapili ,  kiasi  ya watu  21  wameuwawa.

No comments:

Post a Comment