Thursday, January 5, 2012

WASOMALIWA WAKUTWA WAKIWA WAFU

Wahamiaji 20 Wasomali walipatikana wamekufa wiki iliyopita mashariki mwa Tanzania. Duru za polisi zimeeleza jana kuwa huenda walitupwa kichakani kutoka kwenye lori la mfanyabiashara magendo baada ya kukosa hewa  ya kutosha na  kufariki. 
Kamanda wa jeshi la polisi wa mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo amesema wanafanya uchunguzi na kisha hicho  na watatoa  taarifa  baadaye, lakini miongoni mwa waliouwawa ni wanawake watatu. Polisi wamesema wahamiaji hao wanadhaniwa walikuwa njiani kwenda Zambia au Afrika Kusini na walipatikana katika sehemu tofauti kando ya barabara kati ya Desemba 26 mwaka jana na Januari mosi mwaka huu. Maelfu ya Wasomali huikimbia nchi yao iliyokabiliwa na baa la njaa kila mwezi, baadhi wakielekea kambi za wakimbizi katika nchi jirani za Kenya na Ethiopia na wengine kwenda kutafuta ajira katika mataifa mengine kupitia msaada wa wafanyabiashara wa magendo.

No comments:

Post a Comment