Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Mbeya Dokta Mary Mwanjelwa akizungumza na
wananchi wa soko la sido Mwanjelwa jijini Mbeya, ataka watendaji wabovu
kuondolewa ili kuweka heshima kwa serikali.
Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Mbeya Dk
Mary Mwanjelwa akihutubia wananchi katikati ya madimbwi ya maji ya
mvua huku akisisitiza kuwa ataenda kumwona mkurugenzi wa jiji la mbeya
na kumwomba aje afukie madimbwi hayo huku wananchi wakimshangilia kwa
ahadi hizo.
*****
Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Mbeya Dokta Mary Mwanjelwa amehitimisha ziara
yake ya siku nne katika jimbo la Mbeya Mjini, kwa kutembelea kata zote
36 na kuzungumza na wananchi. kupokea kero mbalimbali zinazowakabili
pamoja na mchakato wa katiba.
Akizungumzia
kero ya barabara jijini Mbeya linashughulikiwa kwa ukaribu kwani
Mkandarasi ameshapatikana hivyo barabara ya kilometa 29 za kiwango cha
lami zitajengwa, ili kuondoa adha wanazopata wananchi katika usafiri.
Hata
hivyo amesisitiza wananchi mkoani Mbeya kuwasilisha kero zao kwake ili
kuzifikisha kwa Idara husika, badala ya kukaa na kunung'unika ili
waweze kupatiwa majibu sahihi.
Wakati
huohuo amezitaka tofauti za kisiasa kuwekwa pembeni ili kuijenga Mbeya
yenye mshikamano badala ya kusikia majanga yakiwemo moto na mafuriko
ambayo yamerudisha nyuma maendeleo ya mkoa.
Dokta Mwanjelwa ameongeza kuwa amewataka viongozi kutimiza ahadi zao ili kuleta imani kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment