Sunday, January 15, 2012

MELI YAPINDUKA


DW

Nahodha wa meli ya abiria atiwa korokoroni nchini Italia ,huku uchunguzi ukifanyika juu ya madai ya kuuwa bila kukusudia.

Vyombo  vya  habari  nchini  Italia  vimeripoti   jana  kuwa nahodha  wa  meli  ya  abiria ,inayojulikana  kama  Costa Concordia , ambayo ilipinduka katika  pwani  ya  Toscana , nchini  Italia, ikiwa  na  abiria  4,000  amekamatwa  wakati uchunguzi   unafanyika  juu  ya  madai   ya  kuuwa  bila kukusudia  na  kuitelekeza  meli  yake. 

 

Meli  hiyo  ya  abiria  iligonga  mwamba  baharini  na kusababisha  tundu  la  mita  70  hadi  100  katika  eneo lake  la  mbele , muda  mfupi  baada  ya  kuanza  safari siku  ya  Ijumaa  kutoka   bandari  ya  Civitavecchia  karibu na   Rome. 
Kiasi  ya   watu  42  wamejeruhiwa ,  ambao watu  wawili   hali  zao  ni  mbaya  na  wengine  41  ambao ni  miongoni  mwa  watu  waliokuwa  ndani  ya  meli  hiyo wakiwa  hawajulikani  waliko. 
Meli  hiyo  ilikuwa  ikielekea katika  bandari  ya  Savona  kaskazini-magharibi  ya  Italia na  ilitarajiwa  kusimama  katika  bandari  za  Marseille nchini  Ufaransa  pamoja  na  Barcelona  nchini  Hispania.

No comments:

Post a Comment