Tuesday, December 27, 2011

AUAWA KWA KUFANYA MAPENZI NA MKE WA MTU

Watu wanne wamepoteza maisha katika matukio mawili tofauti mkoani Mbeya likiwemo la mwanaume mmoja kuuawa kwa kutuhumiwa kufanya mapenzi na mke wa mtu.

Jeshi la Polisi mkoani humo limesema tukio la kwanza limetokea  Jumatatu ya Desemba 26, mkazi wa Kabwe jijini Mbeya aliyefahamika kwa jina la Theresia Mbinili (85) alipoteza maisha baada ya gari namba T. 429 AHU aina ya Toyota Hiace kumgonga.

Taarifa hiyo imesema  kondakta wa gari hilo Joshua Laudeni (25) mkazi wa Iyunga amekamatwa na mwili wa marehemu umehifadhiwa  katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, na chanzo cha ajali hiyo  ni kondakta huyo kutosomea udereva na kuendesha bila leseni.

Tukio la pili limetokea Jumatatu ya Desemba 26, mkazi wa Ilongo wilayani Mbarali aliyefahamika kwa jina la Mbatalile Mwakilolile (70) kufa kwa kugongwa na gari namba T 881 BTT aina ya Toyota Hiace katika barabara ya Mbeya-Iringa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo imesema gari hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina moja tu la Sunday, ambaye alikimbia baada ya tukio.

Pia imesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Chimala Mission na kwamba chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi.

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limeongeza kusema, mkazi wa Ifuko wilayani Chunya aliyefahamika kwa jina la Zaina Zawadi (55) amefariki wakati akipatiwa matibabu katika Kituo cha Afya cha Mbuyuni baada ya kupigwa na mwanamke mwenzake.

Imebainika aliyempiga hadi kusababisha kifo chake ni Justa Stephen ambaye amekimbia baada ya kutenda kosa hilo, akimtuhumu marehemu kwa imani za ushirikina  na anatafutwa na Jeshi hilo kwa hatua zaidi.

Katika hatua nyingine Jeshi hilo limesema  mwanaume mkazi wa Chipaka wilayani Mbozi aliyefahamika kwa jina la Amos Siame (37) ameuawa kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali kisha kunyongwa kwa kamba ya gome la mti na kutupwa porini karibu na makaburi ya Chipaka.

Kwa mujibu wa Taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu tukio hilo iliyotolewa  imesema mwili wa marehemu umekutwa na jeraha kubwa shingoni.

Pia imeongeza kusema chanzo cha mauaji hayo ni marehemu kutuhumiwa kufanya mapenzi na mke Jacob Sikaonya (31) mkazi wa Chipaka.

Aidha watu watano wanashikiliwa na Polisi kuhusiana na tukio hilo akiwemo  Frank Sikaonya (28), Nimrodi Sikaonya, Waikunga Sikaonya na Ayub Sikaonya (18).

Imeandikwa na Rester Phares Redio Ushindi FM Mbeya Tanzania Desemba 27, 2011.

No comments:

Post a Comment