Wakristo mkoani Mbeya wametakiwa kuwa na mipango
kwa maisha yao ya baadaye badala ya kutegemea kudra za Mwenyezi
katika mafanikio yao.
Akizungumza katika Ijumaa
ya Marafiki Meneja wa Benki ya Stanbic Tawi la Mbeya Willy Afumwisye amesema
wakristo wengi wamekosa mipango katika maisha yao licha ya Neno la Mungu kuwapa ahadi
kedekede.
Pia amesema wakristo wengi
wamekuwa wakitegemea kuwekewa mikono na Watumishi wa Bwana ili waweze
kufanikiwa kitu ambacho wakati mwingine sio sahihi isipokuwa ni uzembe wa kiakili.
Hata hivyo amesema
kumtanguliza Mungu katika kila jambo ni muhimu sana kwani hakuna mafanikio bila Muumba wa
Mbingu na Nchi na kuongeza kuwa anapopanga ni lazima kupanga na Roho Mtakatifu.
FOF Jijini Mbeya ni ya
Pili, hufanyika kia Ijumaa ya mwisho wa mwezi. Washiriki akali ya 35 walikuwepo
katika Ijumaa ya Marafiki Jijini Mbeya.
Imeandikwa na Johnson Jabir Redio Ushindi
FM Desemba 30, 2011.
No comments:
Post a Comment