Mzozo umeibuka Jijini
Mbeya baina ya madereva wa magari na wamiliki wa vituo vya mafuta kufuatia
wamiliki hao kuzuia mafuta kuuzwa katika vituo vyao kwa siku ya pili sasa.
Uchunguzi uliofanywa na redio Ushindi FM umebaini foleni
kubwa katika baadhi ya vituo vya mafuta Jijini Mbeya kwa magari hayo kutaka nishati hiyo.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyobainishwa na Redio hiyo
yamebaini Kituo cha Mafuta cha JM kilichopo Maghorofani Jijini humo foleni
kubwa ya magari hali ambayo imekuwa tofauti na siku nyingine.
Madereva wa magari hao wamenukuriwa wakisema mrundikano huo
umetokana na EWURA kutangaza bei mpya za nishati hiyo, na kuongeza kuwa
wanaiomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwachukulia hatua
stahili wamiliki hao kwani wanachangia kukwamisha shughuli za kimaendeleo
nchini.
Wamiliki wa vitu hivyo kwa upande wao wameishutumu Mamlaka
husika kutokana na kushusha bei hali ambayo imewaongezea hasara na kuongeza kuwa awali ilikuwa
shilingi 2,200 na sasa ni shilingi 1,800
EWURA huwa na kawaida kila baada ya majuma mawili
kubadilisha bei elekezi ya nishati hiyo kwa kila wilaya nchini Tanzania
kufuatana na umbali kutoka hazina hadi kwa mteja.
* Bei za nishati ya
mafuta katika mkoa wa Mbeya kwa ujumla tangu Desemba 19, 2011
PETROL
|
DIESEL
|
KEROSENE
|
|
MBEYA
|
1989
|
2082
|
2065
|
CHUNYA
|
1999
|
2092
|
2074
|
ILEJE
|
2002
|
2096
|
2078
|
KYELA
|
2005
|
2098
|
2081
|
MBARALI
|
1973
|
2067
|
2049
|
MBOZI
|
1998
|
2092
|
2074
|
RUNGWE
|
1998
|
2091
|
2074
|
*Bei hizi
zimeanza kutumika Jumatatu ya Desemba 19, 2011
|
Moses Mbembela na Rester Pharles Redio
Ushindi FM Desemba 28, 2011
No comments:
Post a Comment